Friday, March 30, 2012
utamaduni halisi wa mwaafrika umeingiwa na kasumba za kigeni
by chacha
Je wajua kuwa miaka nenda miaka rudi utamaduni halisi wa Mwafrika umesambaratika kwa kuingiwa na kasumba za kigeni ambazo kwa hakika haziambatani asilani na mila zetu?
Tukichunguza kwa makini vijana ndio walioathiriwa kupindukia huku maadili yakizorota katika jamii.
Vijana wanaiga desturi za kigeni na kupuuza madhara yake.
Tukipekua kwa kina,kizazi kipya ndicho kinaiga kasumba hizi,ingawa kuna asilimia fulani ya wazazi ambao pia hawataki kuwachwa nyuma.Wasema wataenda sambamba na wakati ingawa hakuna wakati ambao huwa sawia na mwingine.Yanayojiri kwa hakika hayapendezi.
Juzi baadhi ya vijana walihojiwa kuhusu suala hili,mwanafunzi mmoja kutoka katika chuo cha urembo wa nywele alisema kuwa uigaji wa mila na tamaduni za kigeni umefanya bara letu kuitwa bara la giza.
Hii ni kwa sababu vijana wengi wa kiafrika tumekuwa watumwa wa kimawazo na kimaadili.
Tunahesabu itikadi za kigeni kuwa bora kuliko zetu
.Cha maana ni kufurahia mila zetu,maana muacha mila ni mtumwa kama walivyotuasa wahenga.
Sisemi kuiga mila na tamaduni za kigeni ni kosa,lakini tunastahili kuiga mila na tamaduni zilizo na manufaa kwetu.
Hatupaswi kuwa mithili ya bendera ambayo daima dawama hufuata upepo.
Si vibaya kwa vijana wa Kiafrika kwenda sawia na wakati ulivyo ila mila na tamaduni nyingine za kigeni ni fedheha tupu na kashfa isiyomithilika.
Vijana wengine wanapotoshwa kabisa na desturi za kigeni mpaka hawaskii la mwadhini wala la mteka maji kisimani hivyo basi inawabidi kuishi katika dunia yao wenyewe ambapo mwisho huishia katika laiti ningelijua.
Ni jukumu la kila mja katika bara hili teule la Afrika kujifunga kibwebwe na kuhakikisha mia fil mia kuwa itikadi na mila zetu zinakua toka kizazi kimoja hadi kingine kwani majuto ni mjukuu huja kinyume na usipoziba ufaa basi huna budi ila kuujenga ukuta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
شركة مكافحة النمل الابيض بالقصيم
ReplyDelete